BAADHI ya dawa na vifaa tiba zilizotolewa hivi karibuni na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Mhe. Omar Ali Shehe ambazo tayari zimeshapitiwa na muda wake wa matumizi, ambapo uongozi wa hospitali ya Chake chake umezigundua wakati wakitaka kuzitumia.
MWAKILISHI
viti maalumu wanawake CUF wilaya ya Chake Chake, Mhe. Salma Mohamed Ali
(kulia) akimkabidhi dawa na vifaa tiba, Daktari dhamana wa hospitali
ya Chake Chake, Dk. Yussufu Hamad Idd vilivyotolewa na mwakilishi wa
Jimbo la Chake chake, Mhe. Omar Ali Shehe, Mei 3 mwaka huu, kabla ya
baadhi ya vifaa na dawa hizo kugunduilika kupitiwa na muda wake wa
matumizi.
MFAMASIA mkuu wa hospitali ya Chake Chake Pemba, Dk. Kassim Zahir akionyesha vipamba vya kusafisa damu baada ya kung’olewa jino, ambavyo navyo ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyogundulika kupitiwa na muda wake, ambavyo vilitolewa hivi karibuni na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Mhe. Omar Ali Shehe, pamoja na dawa nyengine.
DAKTARI dhamana wa hospital ya Chake Chake Pemba, Dk. Yussuf Hamad Idd, akitoa maelezo jinsi watakavyomkabidhi dawa na vifaa tiba Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake, Mhe. Omar Ali Shehe ambaye hivi karibuni alikabidhi dawa hizo ambazo zimegundulika kupitwa na muda wake wa matumizi.(Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment