Kamera ya mtaa kwa mtaa kama kawaida huku changanyikeni ilifanikiwa kunasa taswirazz kazaa za huduma ya kulisafisha karavati moja korofi mtaani kwetu lililo kuwa likitoa harufu mchanganyiko za kukejeri kutokana na majitaka yaliyo kuwa yametwama chini ya karavati hilo lakini sasa mambo shwari mara baada ya kupigwa msasa na maji yenye kasi na yenye nguvu kutoka kikosi cha zimamoto, maana ilikuwa hata upige manukato ya aina gani lakini ukipita hapa duu.....picha na mtaa kwa mtaa blog.
Gari kutoka kikosi cha zima moto likiwa lina adhibu karavati hilo kwa kutoa maji yenyenguvu kwa njia ya mpira.
Ingawa mpira wa gari hilo umepasuka pasuka lakini ulisaidia kuondoa kiro hiyo mtaani kwetu.
No comments:
Post a Comment