HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 26, 2015

KAMPENI MPYA YA KUHAMASISHA FAIDA NA MATUMIZI YA UZAZI WA MPANGO YAZINDULIWA MKOANI KIGOMA

Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Cosmas Swai, akizindua kampeni mpya ya kuhamasisha Faida na Matumizi ya Uzazi wa Mpango jijini Dar es Salaam jana, kampeni itakayotekelezwa mkoani Kigoma. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la, World Lung Foundation (WLF), Nduke Mwakatundu (mwenye tai) na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk.Leonard Subi (watatu kulia) na baadhi ya wafanyakazi wa (WLF).
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la World Lung Foundation (WLF), Nduke Mwakatundu, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha faida na matumizi ya uzazi wa mpango jijini Dar es Salaam jana, mpango utakaotekelezwa mkoani Kigoma. Kushoto ni Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Dk.Cosmas Swai na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk.Leonard Subi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Leonard Subi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha faida na matumizi ya uzazi wa mpango jijini Dar es Salaam jana, mpango utakaotekelezwa mkoani Kigoma chini ya Shirika la World Lung Foundation (WLF).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad