Ajali mbaya imetokea leo maeneo ya Makunganya, Barabara kuu ya kutoka Morogoro kwenye Dodoma baada ya gari iliyokuwa imewabeba washabiki wa Timu ya Simba Sports Club kupoteza muelekea na kuingia porini, watu nane wamepoteza maisa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya.
Hili ni pigo kubwa sana kwa Timu ya Simba, tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
Globu ya Jamii inatoa pole wa Klabu ya Wekundu wa Msimbazi kuwa kuondokewa na washabiki wake hao, na Mungu aziweke Roho za Marehemu hao mahala pema Peponi, Amin.
Zoezi la uokoaji wa watu waliokuwa ndani gari hilo ikiendelea.
Muonekano wa gari hilo baada ya ajali.
No comments:
Post a Comment