Na. Mwandishi Wetu
Shirika lisilo la Kiserekali la Heifer International limepokea ufadhili wa Shilingi bilioni 1.35 (USD 750,000) kutoka Starbucks Foundation ili kuwasaidia wakulima wadogo wadogo wilayani Mbozi kupitia mradi wa Heifer unaojulikana kama “Mbozi Farmer Livelihood Improvement Project”. Fedha hizi zinatarajia kuziwezesha jumuiya za wakulima wadogo wadogo wa zao la kahawa wa nchi za Afrika Mashariki kuboresha na kuinua viwango vya maisha.
Fedha hizi ni sehemu ya mkakati wa Starbucks wa kujipatia kahawa yenye ubora madhubuti kwa kuwasaidia wakulima wa zao hilo,kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo. Mpaka sasa Starbucks Foundation imechangia jumla ya dola za kimarekani milioni 15 , kwenye miradi mbali mbali ya jamii duniani.Mradi huu utakuwa ni sehemu ya Mradi wa Uendelezaji wa Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD) nchini Tanzania na unatarajiwa kusaidia wakulima wadogowadogo wa kahawa wapatao 5,000.
Heifer na Starbucks walianza kutekeleza miradi pamoja zamani. Mwaka 2009 , baada ya Mkurungenzi Mkuu Howard Schultz kutembelea wakulima wadogowadogo wa kahawa nchini Rwanda; alisikiliza maombi ya wakulima – waliosema kwamba wakipata ng’ombe ; wataweza kupata Maziwa, lishe bora na kipato Zaidi kwa familia zao. Wafanyakazi wa starbucks walikusanyika kutafuta hao ng’ombe kwa ajili ya wakulima wa Rwanda.
Kiasi cha asilimia 90 ya wakazi wa Mbozi wanajishughulisha na Kilimo cha Kahawa. Kadri jinsi bei ya Kahawa inavyoyumba duniani, wakulima wanalazimika kutafuta njia mbadala ya kipato kukidhi mahitaji ya kifamilia ambayo wanashindwa kuyapata kwa kutegemea kahawa tu.
Mradi wetu utazipa baadhi ya familia mitamba na madume ya kupandishia, ili wakulima waweze kujishughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa Maziwa kama njia ya ziada ya kuongeza kipato kwa wakulima wa kahawa na kuwawezesha kujikimu kimaisha. Kwa Wakulima ambao tayari wana fuga ng’ombe wa Maziwa – watapewa mafunzo ya ufugaji bora na mbinu za kufuga kibiashara ili kupata faida. Wafugaji hawa pia watapewa fursa za kukusanya Maziwa kwenye sehemu za kukusanyia Maziwa ili wasindikaji wakubwa waweze kukusanya Maziwa kwa urahisi.
“Kuongeza kipengele cha ufugaji wa ng’ombe wa Maziwa kutahakikisha kwamba wakulima wa kahawa wana kipato cha uhakika ambayo wanaweza kuitumia kuwekeza zaidi kwenye mashamba yao’ alisema Rais na Mkururugenzi Mkuu wa Shirika la Heifer , Pierre Ferrari. ‘ Kuanzisha kipato kinachotokana na ufugaji wa ngombe wa Maziwa kwa wakulima ; kwa hakika kutaongeza mtaji utakaowekezwa kwa pembejeo na teknolojia ya kuongeza uzalishaji wa kahawa.
Mradi huu pia utawawezesha kupata maji salama na vyoo bora ; na pia kuongeza matumizi ya nishati mmbadala.
Mwaka 2014, Starbucks Foundation walitoa Zaidi ya dola za kimarekani Millioni 3.7 kwa mashirika tofauti wanaojihusisha na maendeleo kwenye jamii. Kila wanapowekeza , wanakusudia kuleta maendeleo endelevu kwenye jamii husika, wakibuni miundo mbinu ya kusaidia mabadiliko chanya ya muda mrefu.
Kwa takriban miaka 40 sasa, Starbucks imejikita kusaidia kuboresha familia za wakulima wa zao la kahawa duniani kote. Kwa kupitia mkakati huu maalum wa kujali masilahi ya wazalishaji; Starbucks inalipa bei za kuridhisha, inawezesha wakulima kupata mikopo na misaada ya kitaalam ili kuwasaidia wakulima kumudu changamoto mbalimbali za Kilimo cha kahawa. Kwa miaka 40 iliyopita, Starbucks imewekeza katika miradi shirikishi ya wakulima kufikia kiasi cha dola za kimarekani milioni 70.
No comments:
Post a Comment