Baadhi ya nguo zikichomwa moto baada ya kukutwa na kunguni wengi kupita kiasi.
Taasisi
ya Better Living Aid kupitia kampuni ya Royal Nsyepa General
Supplies ambayo mkurugenzi wake ni Bw Mgalula Fundikira za jijini Dar es
Salaam leo imepeleka mtaalamu wa upulizaji madawa ya kuuwa wadudu kama
kunguni na wengineo katika kijiji cha Amani kilichopo km 6 nje ya mji wa
Tabora.
Hatua
hiyo ya Better Living Aid ilifuatia ombi toka kwa wakazi wa kijiji
hicho chenye wakazi wapatao 70 ambao baadhi yao ni wazee na wenye
uathirika wa gonjwa sugu la ukoma, pamoja na changamoto ya kunguni pia
wakazi wa hao wametoa maombi kwa taasisi hiyo nawasamaria wema wengine
wajengewe vyoo zaidi kwani kwa sasa wana vyoo viwili tu vilivyo kwenye
hali ya kutumika, huku vingine vikiwa vimejaa na haviwezi kunyonyeka.
Akiongea
na mtandao huu mwenyekiti wa kijiji hicho Bw George Lusambilo
alisema"kwa kweli tunaishukuru sana taasisi hii kwa kutuletea msaada
huu, kwani tumekuwa tukilala kwa taabu sana, naona kuanzia leo tutalala
kwa raha kama watu wengine" pia aliongeza "Ila tu jamani msituchoke,
bado tunakumbushia ombi la kujengewa vyoo zaidi kwani idadi yetu na
ukilinganisha na vyoo tulivyonavyo kwa kweli ni changamoto, lakini pia
tunaomba tupate hata ka zahanati kadogo ili mganga na muuguzi wapate
mahala maalum pa kutuhudumia hasa sisi wagonjwa wa ukoma"
Naye afisa ustawi wa jamii mkoa Bw Charles Makoye alisema "kwa niaba ya serikali naishukuru sana tasisi hii ya Better Living Aid
kwa jitihada zao za kuboresha maisha ya wakazi wa hapa kijijni na
napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine
kusaidia kijiji hiki kwani ustawi wa jamii si suala la serikali peke
yake bali ni la jamii nzima inayotuzunguka kwani hawa wazee wametoka
huko huko katika jamii zetu.
Mratibu wa taasisi ya Better Living Aid
ametoa wito kwa makampuni na watu binafsi kuiunga mkono taasisi hiyo
katika jitihada zake za kuwajengea vyoo na zahanati wakazi wa kijiji
hicho. Vile vile ameeleza dhamira ya taasisi hiyo kutafuta wafadhili ili
kujenga zahanati katika kijiji cha Masweya, wilayani Ikungi mkoa wa
Singida alisema "Nilipata kufika kijijini Masweya mapema mwaka huu
ambako nilipata kujua kwamba wakazi wa hapo hulazimika kutembea km 30 na
ushee kwenda kjiji cha Mtunduru kupata huduma za matibabu. Hivyo Better
Living Aid itafanya kila liwezekanalo kijiji hicho kipate zahanati japo
mdogo ya kuweza kuhudumia wagonjwa wa Malaria nk pia zahanati iweze
kutoa huduma kwa wazazi, kitu mambacho kwa sasa hakipo kjijini Masweya.
Shukurani za dhati ziwaendee
Mh Munde Tambwe (viti maalum Tabora), Mh Aden Rageh (Mbunge Tabora
mjini) Bibi Joha Masawe, Bi Mtagwa Fundikira, Bibi Jamila Kaimika, Bibi
Celina Koka na wanachama wote wa kundi la Better Living Aid Tunashukuru kwa msaada wa hali na mali iliyowezesha kijiji cha Amani kufanyiwa fumigation bila kumsahau mtaalamu Bw Selemani Muhogo wa kampuni ya SILVER ENTERTRADE LIMITED aliyepulizia dawa hiyo.
|
No comments:
Post a Comment