Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Halima Dendegu akifungua rasmi semina maalum kwa Maafisa Utumishi kutoka Mikoa ya Lindi la Mtwara Juu ya Maendeleo ya Mfuko wa Pensheni wa GEPF,uliofanyika Mkoani Mtwara.Katika hotuba yake ya Ufunguzi,Mh. Dendegu ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mfuko wa GEPF kwa kuifikisha elimu hiyo katika mikoa hiyo ya kusini.
Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF,Bw. Aloyce Ntukamazina akiwasilisha mada juu ya maendeleo ya Mfuko wa GEPF, mafao mapya yatolewayo pamoja na faida za kuwa mwanachama,wakati wa semina maalum kwa Maafisa Utumishi kutoka Mikoa ya Lindi la Mtwara.
Afisa Utumishi kutoka wilaya ya Kilwa,Bw. Masimba akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wenzake mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo maalum.
Mmoja wa Washiriki wa Semina hiyo akitoa ushauri kwa uongozi wa Mfuko wa GEPF mbele ya Mkuu wa Mkoa.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF Mkoa wa Mtwara,Bw. Deogratias Kakoko aliyeketi kushoto kwa Mkuu wa Mkoa wakisikiliza kwa makini ushauri uliotolewa na washiriki wa semina hiyo.

No comments:
Post a Comment