Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) yakabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mafuriko Kahama. Msaada uliotolewa ni pamoja na mchele kilo 740, unga kilo 600, maharage kilo 300 na mafuta ya kupikia lita 260.
Msaada huo umekabidhiwa na Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt. Kamugisha Kazaura.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa TTCL Bw. Peter Kuguru alisema TTCL inawapa pole sana wahanga wa tukio hilo na kwamba TTCL imepokea kwa huzuni kubwa tukio hilo na kuwataka Watanzania kuwaombea waliopatwa na janga hilo wapate faraja na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu waliopoteza maisha awapumzishe mahali pema peponi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe.Benson Mpesya akizungumza baada ya kupokea msaada huo, aliishukuru TTCL kwa kuona umuhimu wa kuwafikia wahanga wa mvua hiyo na kuongeza kuwa TTCL wamekuwa na moyo wa huruma kwa wahanga hao huku akiahidi kuwa misaada inayotolewa na watu wenye mapenzi mema itatumika kwa wahanga wa tukio hilo na si vinginevyo na atakuwa mkali kwa hilo.
Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mafuriko Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya (Kushoto) akipokea msaada kutoka kwa Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru(Kulia).
Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru (Kulia) akikabidhi msaada kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya (Kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akitoa neno la shukhurani baada ya TTCL kukabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mafuriko Kahama.
Wananchi wakiongozwa na Kundi la Scout wakishusha msaada wa chakula kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yaliyotokea wilayani Kahama hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akizungumza na Wafanyakazi wa TTCL mkoa wa Shinyanga .







No comments:
Post a Comment