HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 15, 2015

KWA MTINDO HUU,MIZINGA HAITAISHA NCHI HII

 Kamera ya Mtaa kwa Mtaa katika pita pita zake,ililinasha tukio hili la magari yaliyokuwa yakivutana bila ya tahadhali,na kiukweli alichokifanya dereva wa gari ya mbele inayoivuta nyingine si kitu salama kabisa.alifahamu fika anakoingia ni kwenye barabara kubwa inayoruhusu magari kwenda kasi,lakini yeye akijiinginza na kumuacha mvutwaji akiwa kasimama katikati ya barabara huku yeye akiwa kajiweka sehemu ambayo ni salama kwake lakini si salama na ukiangalia kwa makini utabaini dereva wa gari inayovutwa ametoa mkono nje kwa lengo la kuzuia gari lolote linalokuja kitu ambacho hakiwezekani kwa mwenye akili ya kawaida.Kiukweli kabisa wazee wa Feva wanatakiwa kufanya kazi kubwa sana kuhakikisha uzembe wa namna hii hautokei tena na hatuombei mabaya,lakini lolote laweza kutokea kutokana na uzembe wa hivi.hii imetokea maeneo ya Tabara Alhamza kama unaelekea Buguruni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad