Kamera ya Mtaa kwa Mtaa mchana huu imekutana na tukio hili la ajali iliyohusisha Gari dogo aina ya Vitz na Pikipiki maarufu kama Bodaboda katika barabara ya Soko Matola inayoelekea Stendi kuu ya Mabasi,Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa.Ajali hii imetokana na uzembe mkubwa wa Dereva wa Bodaboda ambaye alikuwa akitaka kuipita gari hii iliyokuwa tayari imeonyesha ishara ya kukatisha upande wa kushoto,lakini kutokana na haraba alizokuwa nazo mwendesha boda boda huyo aliamua kutaka kupita na hapo ndipo mambo yakawa namna hii.Mwendesha bodaboda huyo alipobaini kuwa yeye ndio mwenye makosa aliruka kutoka kwenye pikipiki yake hiyo na kutokomea kusikojulikana.
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio huku wakiendelea kujadiliana juu ya tukio hilo.



No comments:
Post a Comment