HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 21, 2014

MAONYESHO YA SABA YA MAGARI YAZINDULIWA JIJINI DAR

Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odilo Majengo (katika) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua maonyesho ya Saba ya Magari yajulikanayo kama Autofest jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Biafra.kulia ni Msaidizi Binafsi wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Deodatus Timothy Ndunguru na kushoto ni Mratibu wa maonyesho hayo Bw. Ally Nchahage.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika banda la Jaffarais Car Wash wakisubiri wateja kwa ajili ya kuwaoshea magari ikiwa ni mchango kwa ajili ya kusaidi wagonjwa walioko hospitali ya Taifa Muhimbili watokanao na ajari za barabarani. Tukio hili limefanyika jana katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Msanii Singo Mtambalike aka Rich Rich (aliyeshika mpira wa maji) na msanii wa kike Bi. Kajala Masanja ( aliyeshika ndoo) wakiosha gari la mteja aliyefahamika kwa jina la Furaha Mansoor (hayupo pichani) mara baada ya kufikia makubaliano ya kumuoshe gari mteja kwa ikiwa ni mchango wa kusidia wahanga wa ajari za barabarani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wasanii hao waliosha gari hilo kwa gharama ya shilingi laki tano za kitanzania.
Mkurugenzi waKampuni ya SBP Bw. Furaha Mansoor (katikati) akiwakatika picha yapamoja na wasanii Singo Mtambalike aka Rich Rich (kushoto) na Kajala Masanja (kulia) mara baada ya wasanii hao kumaliza kumuoshea gari lake wakati wa maonyesho ya magari na zoezi la uchangiaji wa hiari kwa wahanga wa ajari za barabarani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Biafra
Wasanii Johari Chagula (anayepaka sabuni) na Monalisa ( aliyeshika mpira wamaji) wakiosha gari la mteja aliyefahamika kwa jina la Feisar (hayupo pichani) mara baada ya kufikia makubaliano ya kumuoshe gari mteja huyo kwa ikiwa ni mchango wa kusidia wahanga wa ajari za barabarani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akifurahia zawadi ya Kikombe aliyopewa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Kuunganisha wauzaji na wanunuzi wa magari Tanzania kupitia mtandao wa cheki.co.tz Bw. Mori Bencus jana jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ndiyo wadhamini wakuu wa maonyesho hayo ya saba ya Autofest ambapo wameingia kwa mara ya kwanza katika biashara hapa nchini Tanzania mwaka 2014 wakiwa na lengo la kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora na kwa wakati.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mahusiano wa Bank ya Afrika Tawi la Tanzania (BOA Bank) Bi. Gereta Gonga alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo jana jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija, MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad