HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 24, 2014

Yassin Abdalla (Ustaadh) awa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA)

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) katika kikao chake kilichokaa tarehe January 4, 2014 jijini Kigali, Rwanda, limefanya mabadiliko ya kujaza nafasi za uongozi.

Yassin Abdalla (Ustaadh) wa Tanzania ameteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa ECAPBA. Abdalla ambaye ni Rais wa TPBO amejaza nafasi ya Celestino Mindra wa Uganda aliyekuwa Rais wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa ya Uganda (UPBC)

Simon Kategole wa Uganda, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa ECAPBA kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Shaban Ogolla wa Kenya ambaye yuko masomoni nchini Marekani. Daudi Chikwanje wa Malawi anachukua nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa ECAPBA.Aidha, Nelson Sapi wa Zambia ameteuliwa kuwaNaibu Mweka Hazina wa ECAPBA akimsaidia Nemes Kavishe wa Tanzania.

Bonifawa Wambura wa Tanzania anabaki kuwa Afisa Habari wa ECAPBA wakati wajumbe wanne wameongezwa kwenye Kamati ya Utendajji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Malawi na Ethiopia pamoja na Roman Chuwa wa jiji la Arusha.

Aidha, ECAPBF inamshukuru Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwa kukubali kuwa mlezi wake na kuipatia ofisi katika Manispaa ya jiji la Arusha ikikumbukwa kwamba ndicho chombo cha kuwaunganisha vijana cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Katika malengo yake, ECAPBA itafanya kazi kwa karibu sana na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) ili iweze kuwa chachu ya utekelezaji wa maamuzi ya Jumuiya katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati.

Kwa kutambua kuwa, Jumuiya ya Afrika ya Mashariku ni chombio cha uchumi cha kuunganisha nguvu za watu wa Afrika ya Mashariki, ECAPBA imedhamiria kuyafanyia utekelezaji maamuzi yote yanayohusu maendeleo ya vijana pamoja na ushirikiano wa utamaduni na michezo wa EAC. Aidha, ECAPBA imedhamiria kuleta chachu katika kujenga nguvu na kutengeneza ajira kwa vijana wa Afrika ya Mashariki na Kati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad