HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 24, 2014

WAZIRI WA FEDHA WA TANZANIA AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA WA ZANZIBAR NA VIONGOZI WA WIZARA HIZO HUKO ZANZIBAR

Waziri wa Fedha wa Zanzibar,Mh. Omar Yussuf Mzee (wa pili kulia) akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar katika mkutano wa kuimarisha Umoja na mashirikiano ya ukaribu baina ya Wizara ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Fedha ya Zanzibar. katika Ukumbi wa  Hoteli ya Serena Inn Shangani Mjini Zanizbar.kulia kwake ni Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mh. Saada Mkuya na mwengine ni Naibu Waziri wa Fedha wa Tanzania,Mh. Mwigulu Nchemba na wakwanza kulia ni Naibu Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mh. Adam Malima.
Waziri wa Fedha wa Tanzania,Mh. Saada Mkuya (wapili kushoto) akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Fedha ya Tanzania na Zanzibar katika Mkutano wa kuimarisha Umoja na mashirikiano ya ukaribu katika Hoteli ya Serena Inn Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Fedha wa Tanzania,Mh. Saada Mkuya katikati akipokea zawadi ya Mlango na makubadhi vyenye historia ya zanzibar mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuimarisha Umoja na mashirikiano ya ukaribu katika Hoteli ya Serena Inn Shangani Mjini Zanzibar.kushoto yake ni Waziri wa Fedha wa Zanzibar,Mh. Omar Yussuf Mzee na kulia yake ni Naibu Waziri wa Fedha wa Tanzania,Mh. Mwigulu Nchemba .
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika Mkutano wa kuimarisha Umoja na Mashirikiano baina ya Wizara ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Fedha ya Zanzibar. katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Inn Shangani Mjini Zanizbar.
Waziri wa Fedha wa Tanzania,Mh. Saada Mkuya wapili kulia na Waziri wa Fedha wa Zanzibar,Mh. Omar Yussuf Mzee katikati wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Fedha ya Tanzania na Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuimarisha Umoja na mashirikiano ya ukaribu katika Hoteli ya Serena Inn Shangani Mjini Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad