MKurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd,inayoandaa tamasha la Krismasi,Bwa.Alex Msama akizungumza
na baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar
jana wakati alipokuwa akielezea maandalizi ya lala salama ya tamasha
hilo,linalotarajiwa kufanyika siku ya sikukuu ya Krisimasi,kwenye Uwanja
wa Taifa.
Tamasha
hilo litakalojumisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za kiroho wa hapa
nyumbani sambamba na kutoka nje ya nchi ikiwemo nchini Afrika Kusini na
Rwanda.Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho kutoka nchini Afrika
Kusini,Solly Mahlangu na Liliani Kabaganza kutoka nchini Ruanda
wanatarajiwa kuwasili jijini Dar leo tayari kwa ushiri wa tamasha hilo
linalowakutanisha watazamaji lukuki.
Msama aliwataja baadhi ya Waimbaji watakatumbuiza kwenye tamasha hilo la Krisimas,kuwa ni Rose Muhando,Solomon Mukubwa,Upendo Nkone,Upendo Kilahiro,Anastazia Mukabwa,John Lissu,Boni Mwaitege,Ephrahim Sekeleti,Glorious Warship Team,The Voice Acapella,New Life Band na wengineo kibao.
Msama alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekwishakamilika na kinachosubiriwa mashambulizi tu yatakayoanzia jijini Dar,Morogoro,Tanga,Arusha na kumalizia mkoani Dodoma


No comments:
Post a Comment