Katika barabara ya Jamhuri pembeni ya jengo refu la Benjamin Mkapa Tower, maeneo ya katikati ya jiji letu pendwa la Dar es Salaam kuna hiki kipita shoto kama kionekanavyo pichani hapa.Kiukweli kabisa kipita shoto hiki kimedumu kwa majuma kadhaa sasa bila ya kupambwa kwa maua na majani kama tuonavyo kwenye vipita shoto vingine vingi hapa nchini, yaani ni Kama kimechuniwa hivi.sasa Swali langu kwa wahusika, hivi ni kwamba mmekidharau kipita shoto hiki ambacho kinaonekana ni bora na chenye mvuto kwa macho ya watu ama ni nini???
Hivi ndivyo kionekanavyo kipita shoto hicho kwa karibu, kiukweli kinavutia sana



No comments:
Post a Comment