Waandishi wa Habari kutoka Tanzania na Kenya wakimsikiliza Muongozaji wa Watalii katika Makumbusho ya Hector Pieterson (Mtoto aliekufa kwa kupigwa risasi wakati wa kutafuta haki ya Mwafrika nchini Afrika Kusini) aitwae Antoinette Sithole (kulia) ambaye pia ni Dada wa Hector Pieterson na wanaonekana kwenye picha ya chini hapo wakikimbia.Aliembeba Hector alitambulika kwa jina la Mbuyisa Makhubo ambaye hajulikani alipo mpaka leo hii toka siku hiyo.Hector Pieterson na Antoinette Sithole wote walikuwa ni Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Phefeni,iliopo Orlando West, Soweto,Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.Waandishi hao wapo nchini Afrika Kusini kwa Ziara ya kutembelea vivutio mbali mbali vilivyopo nchini humo kwa Mualiko wa Bodi ya Utalii ya Afrika Kusini.
Hii ndio picha pekee yenye Kumbukumbu ya Hector Pieterson akiwa amebebwa na Mbuyisa Makhubo huku wakikimbia pamoja na Dada wa Hector aitwae Antoinette Sithole.Picha hii ilipigwa na Mpiga Picha maarufu wa Johannesburg newspaper The World,Sam Nzima.
Dada wa Hector Pieterson ambaye kwa sasa anafanya kazi ya katika Makumbusho hayo,Antoinette Sithole (wa pili kulia) akitoa maelezo ya kumbukumbu yake siku mdogo wake alipopigwa risasi mnamo mwaka 1976,wakati huo yeye alikuwa na umri wa miaka 17.Wanaomsikiliwa toka Kulia ni Othman Michuzi,Pumla Dabula (kutoa Bodi ya Utalii wa Afrika Kusini) pamoja na Anganile Mwakyanjala.

Jiwe la msingi la Kumbukumbu ya Hector Pieterson.
Picha ya Pamoja.
Sehemu ya Watalii kutoka nchini mbali mbali wakisubiri kuingia kwenye Nyumba aliyowahi kuishi Rais wa kwanza wa nchi ya Afrika Kusini,Mzee Nelson Mandela iliopo kwenye Mtaa wa Vilakazi,Orlando West, Soweto,Jijini Johannesburg kwa ajili ya kujionea kumbukumbu za Rais hiyo wakati wa kuutafuta Uhuru wa nchi hiyo.
Meneja wa Kukuza Biashara wa Kampuni ya Frontline,Hellen Kiwia (kati) akiwa na Mwandishi wa Habari,Susan Wong (kulia) kutoka Kenya pamoja Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Frontline,Suleiman Khamis wakipata picha ya pamoja nje ya nyumba ya Mzee Mandela,ilipo kwenye Mtaa wa Vilakazi,Orlando West, Soweto,Jijini Johannesburg.
Kina sie pia hatukutaka kupitwa na taswira hii ya nyumba ya Mzee Mandela,hapa nikiwa na Mdau Atuza Nkurlu ambaye ni Mwandishi wa Gazeti la The Guardian la Tanzania.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Bibi Madona ambaye ni Mtembeza Watalii ndani ya Nyumba ya Mzee Mandela.
Wadau Frank Amani na Suleiman Khamis wakiangalia picha mbali mbali za historia zilizopo ndani ya nyumba hiyo.
Mie nikiwa pembeni ya picha ya Mzee Mandela.
Moja ya picha ya Mzee Mandela akiwa na Familia yake.
Ujumbe wa Mzee Mandela ndani ya nyumba hiyo.
Mgahawa wa Familia ya Mandela.
No comments:
Post a Comment