HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 11, 2013

RAIS KIKWETE ZIARANI MKOANI GEITA LEO

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwika ndoo ya maji Bibi Asha Ahmadi kutoka katika kijiji cha Shinyanga A wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji wa Nyakafuru ulofanyika katika kijiji cha Shinyanga A,Wilayani Mbogwe, Mkoani Geita leo asubuhi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsabahi mtoto Pascal John aliyelazwa katika kituo cha afya Iboya Wilayani Mbogwe wakati  alipozindua Wodi ya akina mama leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi mradi wa Umeme Katoro,Mkoani Geita leo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

1 comment:

  1. Othman mimi huwa napitiapitia blogu yako na asante kwa kutuhabarisha. Kama unajua washauri wa mhe rais JK naomba uwaeleze kwamba wamshauri yeye pamoja na viongozi wengine waache huu mtindo wa kuwatwisha ndoo za maji akina mama wakati wanapoashiria uzinduzi wa visima vya maji. Inabidi tufike mahala tuoneshe kwamba na sisi tunabadilika kutoka fikiri za kijima na kuwa wabunifu. Kuwatwisha ndoo akina mama katika karne ya 21 si ishara nzuri kwa akina mama wenyewe wala jamii kwa ujumla na sio kitu cha kujivunia kiasi cha kufanywa na Rais. Ningependekeza, wanapokuwa wanaandaa shughuli za uzinduzi kama hizi watengeneze angaa kigari cha kusukuma ambacho kinaweza kubeba ndoo kama mbili. Anapoashiria uzinduzi ionekane ama mama au hata baba akijaza maji kwenye hizo ndoo zilizo kwenye kigari. Hii itakuwa njia mojawapo ya kuhimiza fikira za kuwapunguzia mzigo akina mama - badala ya kubeba ndoo kichwani, wanasukuma mkokoteni. Ndiyo, maendeleo kutoka ujima kwenda kwenye usasa yalianza na ugunduzi wa gurudumu. Tubadilike katika fikira na vitendo pia.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad