Mery Kanyaga, akimpongeza binti yake, Shelder Boniface ambaye ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ muda mfupi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, wakitokea Msumbiji katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Dunia za wanawake ambako Tanzanite iliichapa Msumbiji mabao 5-1 huku Shelda akitupia matatu kati ya hayo.
Wachezaji wa timu ya taifa ya wananwake chini ya umri wa miaka 20 'Tanzanite' wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Msumbiji katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la Dunia la wanawake dhidi ya Msumbiji, ambako Tanzania ilishinda 5-1.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘The Tanzanite’ wakiwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakitokea Msumbiji katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Dunia za wanawake ambako Tanzanite iliichapa Msumbiji mabao 5-1.

No comments:
Post a Comment