Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi rasmi wa Mbio za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Machi,201 huko Mkoani Kilimanjaro.Uzinduzi huu umefanyika mapema leo asubuhi katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower,Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ndio Wadhamini Wakuu wa Mbio hizo,George Kavishe akizungumza machache namna walivyojipanga kufanyikisha mbio hizo ikiwa ni Mwaka wa 12 sasa tangu kuanza kudhamini mbio hizo.
Mratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marathon,Aggrey Mareale akizungumza katika uzinduzi huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini,Suleiman Nyambui akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Mbio za Kilimanjaro Marathon mwaka 2014.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akikabidhi Bendera ya Mbio za Kilimanjaro Marathon kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini,Suleiman Nyambui (kulia) mara baada ya uzinduzi huo.Wengine pichani ni Wadhamini wa Mbio hizo.
Waandishi wa habari wakichukua tukio hilo.







No comments:
Post a Comment