Hii ndio ndege pekee aina ya McDonnell Douglas MD-83 inayozunguka la Kombe la Dunia la Fifa katika nchi mbali mbali Duniani,na leo Kombe hilo lipo jijini Dar na tayari mambo yameanza kupamba huko Uwanja wa Taifa kwa kuwawezesha watu mbali mbali kuweza kuliona na kupiga nalo picha.Burudani mbali mbali zitatolewa leo kwenye Uwanja huo wa Taifa.
Mie nikizama ndani ya pipa hilo libebalo Kombe lenye hadhi kubwa Duniani kote,hapa tukitokea jijini Nairobi nchini Kenya jana kuja Tanzania.je wataka kujua nilikuwa kwenye safari hii kama nani????
Msanii wa Muziki kutoka nchini Brazil,David Correy (kulia) akiwa na DJ wake ndani ya Ndege hiyo wakati wa Safari ya kutoka Jijini Nairobi nchini kwenye kuja Tanzania.David Correy ndie Balozi Coca - Cola ambaye anatumbuzi kwenye kila Tamasha la Maonyesho ya Kombe hilo Duniani kote.
Mie nikiwa na Dada Waithera Kabiru ambaye ni Meneja Masoko wa Kidigita (Digital Marketing Manager) wa Kampuni ya Coca-Cola nchini Kenya,wakati wa Safari yetu ya kutoka Jijini Nairobi kwenda Mwanza.
Wadau ndani ya Dege hilo.
Nchi ambazo Kombe hilo litapita kama zionekanavyo ndani ya Ndege hiyo.








No comments:
Post a Comment