Wakimbiza kuku ambao ni mashabiki wa Simba, Salage Mbulanzu na wa Yanga Anastella Elias wakipigwa bonge moja la chenga na Kuku wanaemkimbiza wakati wa Bonanza la ‘Nani Mtani Jembe’ lililofanyika kwenye uwanja wa Namfua wa mkoani Singida. Kuku huyo alichukuliwa na shabiki wa Simba.
Mashabiki wa Simba na Yanga wakishindana kuvuta kamba wakati wa bonanza la ‘Nani Mtani Jembe’ lililofanyika kwenye uwanja wa Namfua ulioko mkoani Singida mwishoni mwa wiki, Simba walishimba mchezo huo. Bonanza hilo lilidhaminiwa na kuandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Mashabiki wa Simba na Yanga, Igos Abdallah na Seif Omar wakishinda kukimbia na magunia kwenye mchezo huo wa kupokezana wakati wa bonanza la ‘Nani Mtani Jembe’ lililofanyika kwenye uwanja wa Namfua ulioko mkoani Singida mwishoni mwa wiki.
Mkimbiza kuku wa mashabiki wa Simba, Salage Mbulanzu akimkata kuku huku Anastella Elias akiwa hana la kufanya wakati wa bonanza la ‘Nani Mtani Jembe’ lililofanyika kwenye uwanja wa Namfua wa mkoani Singida.
Mchezaji wa timu ya mashabiki wa Simba kwa wanawake, Mwile Simon akikimbia na mpira wakati beki wa mashabiki wa Yanga, Anastella Elias akijiandaa kuzuia hatari isitokee golini kwake kwenye bonanza la mashabiki wa timu hizo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Namfua wa mkoani Singida, kushoto ni, Salage Mbulanzu. Simba ilishinda 1-0.







No comments:
Post a Comment