Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuzindua ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Mkoa wa Kipolisi Temeke. Kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa
Askari na Maofisa wa Jeshi la Polisi, Viongozi wa Mashirika na Taasisi
zisizo za Serikali pamoja na wakazi wa Temeke kabla ya kuzindua Mpango
Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto
ndani ya Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilifanyika Kituo cha Polisi
Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP) Said Mwema. Waziri Nchimbi akatika hotuba yake
alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi
zisizo za Serikali kwa kusaidia masuala ya kupambana na unyanyasaji wa
kijinsia nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikionyesha kitabu cha
Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na
Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha
Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wapili kushoto ni Balozi wa
Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Waziri Nchimbi akatika hotuba yake alilishukuru Jeshi la Polisi pamoja
na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali kwa kusaidia
masuala ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia nchini.

.jpg)


No comments:
Post a Comment