HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 4, 2013

Wabunge 7 wajiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Dk. Aggrey Mlimuka (kushoto) akimkabidhi kadi ya Uanachama wa PPF,Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii na Mbunge wa Jimbo la Peramiho,Mh. Jenista Mhagama muda mfupi baada ya kujiunga na Mfuko huo,ambapo zaidi ya Wabunge Saba walijiunga na Mfuko huo.Makabidhiano hayo yalifanyika jana jioni kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha kunakofanyika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Dk. Aggrey Mlimuka (kushoto) akimkabidhi kadi ya Uanachama wa PPF,Mbunge wa Viti Maalum,Mh. Amina Mwidau muda mfupi baada ya kujiunga na Mfuko huo,ambapo zaidi ya Wabunge  saba walijiunga na Mfuko huo.Makabidhiano hayo yalifanyika jana jioni kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha kunakofanyika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio.
 Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni,Mh. Habib Mnyaa akijaza Fomu za kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF,wakati wa Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mbunge wa Jimbo la Singida kusini,Mh. Mohamed Misanga pia alikuwa ni mmoja wa Wabunge hao waliojiunga na Mfuko huo wa PPF.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad