HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 16, 2013

Waziri Mwakyembe awafukuza kazi wale wote waliohusika kusaidia kusafirisha madawa ya kulevya

Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Uchukuzi juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko Afrika Kusini hivi karibuni.Dkt. Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa hayo, pia Waziri Mwakyembe ameliagiza jeshi la Polisi kuwakamata wafanyakazi hao na kuwaunganisha na wenzao kujibu mashitaka ya jinai.
Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akionyesha picha ya Msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari,masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko nchini Afrika Kusini hivi karibuni.
waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Uchukuzi akiwa anafafanua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuushughulikia mtandao mzima uliosaidia kupitisha madawa ya kulevya.

1 comment:

  1. Sawa Mheshimiwa Dr.Mwakyembe amethubutu. Lakini ni kweli kwamba hawa dagaa hawa wanafanya wenyewe? Ni kweli kwamba hakuna papa katika watawala tulio nao? Je! huyo mtu anayesemekana alikuwa akiongea kwa simu muda wote wale watu walipokuwa wakipitisha huo unga alikuwa anaongea na nani? Je!, Dr Mwakyembe anaogopa kumtaja huyo kigogo mkuu kabisa wa unga kwa sababu ana mamlaka kuliko yeye? Je!, Dr.Mwakyembe kaficha taarifa zingine kama alivyoficha zile za Richmond? Je! hao watu wa usalama wa taifa hatima yao ni ipi? Na mheshimiwa Stephen Wasira anasemaje kuhusu hao watu kwa kuwa wako chini ya himaya yake? Au yeye mwenyewe ndiye kigogo mkuu? Na mkuu wa usalama wa taifa anasemaje kuhusu watu walioko chini yake? Kujishughulisha na madawa ya kulevya ni sehemu ya kazi za usalama wa taifa?.Mimi nadhani kuna matatizo mahali fulani. Kama tunataka kuondokana na matatizo haya tunatakiwa kuwa wawazi kabisa. Pale inapobidi tuwe tayari kuwajibika hata kama ina maanisha kujiuzulu

    ReplyDelete

Post Bottom Ad