HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 5, 2013

WATEJA WA MAJI MUWSA SASA KULIPA ANKARA ZAO KWA NJIA YA MTANDAO

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)Cyprian Luhemeja akizungumza na wanahabari katika ofisi za bodi ya mamlaka hiyo.
Afisa uhusiano wa mamlaka ya mai safi na maji taka mjini Moshi Dollah Kilo akimfuatilia mkurugenzi wa mamlaka hiyo Cyprian Luhemeja(hayuko pichani)kulia kwake ni afisa mapato wa mamlaka hiyo Brucevictor Sangawe.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro wakimfuatilia mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi (MUWSA) Cyprian Luhemeja(Hayuko pichani)
Wafanyakazi wa kitengo cha habari na mawasiliano wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA) wakimsikiliza mkurugenzi wa mamlaka hiyo Cyprian Luhemeja(hayupo pichani)

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi

ZAIDI ya wateja 21,000 wa mamlaka ya majisafi na taka mjini Moshi(MUWSA), wanatarajiwa kuanza kulipia Ankara zao za maji kwa kutumia mitandao ya Tigo Pesa, M-PESA ,Airtel Money na Eazy Pesa kuanzia mwezi septemba mwaka huu.

Mamlaka kuingia katika mitandao hiyo imelenga kuwarahisishia wateja wake muda wa kukaa katika foleni kwenye ofisi za mamlaka na sasa watapata fursa ya kufanya shughuli zao za kiuchumi na kuongeza uzalishaji mali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,mkurugenzi mtendaji wa MUWSA, Cyprian Luhemeja alisema mpango huo aliouita wa 'Dijitali' upo katika hatua za mwisho na ni sehemu ya uboreshaji wa huduma kwa wateja na kuongeza ufanisi katika shughuli za maendeleo.

Alisema pamoja na mpango huo,hautaathiri nafasi za ajira kwa watumishi wake bali wanachofanya kwa sasa ni kusimamisha ajira mpya na waliopo kuhamishiwa katika ofisi ndogo ya Himo ambayo ni sehemu ya mamlaka itakayokuwa ikitoa huduma.

Mapema wakati wa ziara yake ya siku nane mkoani Kilimanjaro,naibu waziri wa maji Dk Binillith Mahenge aliitaka MUWSA kusaidia usambazaji huduma ya maji katika mji mdogo wa Himo ikiwa ni baada ya kutoridhishwa na usambazaji unaofanyika sasa.

Akizungumzia mgawo wa maji,Luhemeja alisema umefutwa baada ya mamlaka kufanikiwa kupunguza upotevu wa maji wa asilimia 39 hadi kufikia asilimia 28 mapema mwezi uliopita huku lengo likiwa kufikia asilimia 9 ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

“Chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa ‘Big result now’ hakuna tena mgawo wa maji kuanzia Agosti 1, tumefungua call center,wateja watatupigia simu kupitia namba ya bure 0785 555555,nyingine 02755045 au 0275500021 saa 24,kueleza matatizo ya maji katika maeneo yao”alisemaLuhemeja.

Aidha mkurugenzi huyo alisema bado kuna upungufu wa maji kwani kiasi kinachozalishwa sasa ni lita za ujazo 27,000 huku mahitaji ni uzalishaji wa lita 38,000 na kwamba lengo ni kuzalisha lita za ujazo 40,000.

Alisema kiwango cha maji kitaongezeka mara baada ya kukamilika kwa Visima vya Lunguo, KCMC na tanki la Kilimanjaro,huku pia mamlaka ikitenga zaidi ya Mil 46 kwa ajili ya usambazaji maji maeneo ya Kiborloni, Rau na KDC.

Kwa upande wake,afisa uhusiano wa mamlaka hiyo,Dora Killo alisema mamlaka hiyo ina zaidi ya wateja 21,000 katika manispaa yaMoshi,sehemu ya weruweru na Shirimgungani wilayani Hai na baadhi ya maeneo wilayani Moshi vijijini huku lengo likiwa kufikisha wateja 50,000 ifikapo Juni mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad