Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Gregory G Teu akiongozwa na Mkurugenzi wa Mipango Mkakati na Uhusiano wa Kibiashara wa benki ya TIB Jaffar Machano kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na TIB wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda hilo katika maonesho haya ya NaneNane.
Mkurugenzi
wa Mipango Mkakati na Uhusiano wa Kibiashara wa benki ya TIB Jaffar
Machano akimuonesha Kamishna wa Polisi Mkoa wa Dodoma baadhi ya bidhaa
zinazozalishwa na wawekezaji waliokopeshwa na benki ya TIB waliopo ndani
ya Banda la TIB.
Mheshimiwa Mbunge wa Kondoa kusini Juma Nkamia akipata maelezo juu ya moja ya huduma zinazotolewa na benki ya TIB mara baada ya kutembelea banda la TIB katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea Mkoani Dodoma. Benki ya TIB ni mdhamini mkuu wa Maonesho haya.
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la TIB wakiwa katika darasa maalumu ndani ya banda hili kwa ajili ya kuwapatia wananchi maelezo ya jinsi gani ya kunufaika na huduma za kibenki na kuwaongezea ujuzi wa kibiashara. Madarasa haya hutolewa kila siku bandani hapo.

No comments:
Post a Comment