Na Ali Issa- Maelezo Zanzibar
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan amewataka Maafisa Uhamiaji wanao kusanya Mapato kuwa waadilifu katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na huduma wanazo zitoa hapa nchini ili kuweza kujitatulia changamoto zinazo wa kabili.
Hayo ameyasema leo huko katika Ofisi ya Uhamiaji Kilimani mjini Unguja wakati alipofanya Ziara ya kuitembelea Idara hiyo ikiwa ni mfululizo wa Ziara zake ya kuzitembelea Taasisi za Muungano zilizopo Zanzibar.
Amesma iwapo Maafisa hao watafanya kazi kwa uadilifu katika kukusanya Mapato wataweza kuzitatua changamoto zinazo wakabili katika idara yao na kupiga hatua mbele.
Aidha waziri huyo alisema kuwa iwapo uadilifu utaongezwa matatizo madogo madogo kama vile uchimbaji wa Kisima na Ufungaji wa Lifti katika Jengo jipya la Uhamiaji ni rahisi Maafisa hao kuufanya wenyewe ndani ya kipindi kifupi.
Waziri huyo aliwaeleza wafanyakazi hao kulifanyia kazi suala hilo pamoja na kuwa na mashirikiano katika kazi na maamuzi wanayoyatoa yawe ya pamoja bila ya kuwa na malumbano.
Awali akimkaribisha Waziri Samia, Kamishna wa uhamiaji Zanzibar Mwichum Hassan Salum amemueleza waziri kuwa katika kuleta uadilifu wa ukusanyaji wa mapato Idara ya uhamiaji imeunzisha Kitengo kinachopambana na rushwa kwenye huduma zao.
Mwichumu alimueleza Waziri kuwa Idara hiyo inakabiliwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa watumishi 105 ambapo kwa sasa idadi ni Watumishi 375 ambao ni wa chache kutokana na majukumu kuongezeka.
Katika hatua nyingine Waziri Samia alitembelea idara ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ofisi ya Zanzíbar na kuwasihi Watendaji wake kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na uzalendo na bila kumpa mtu yetote asiyestahiki kitambulisho hicho.
No comments:
Post a Comment