Wagombea wa nafasi za ujumbe wa baraza la Marekebisho ya Katiba kutoka Mta wa Oysterbay Kata ya Msasani jijini Dar es Salaam, wakipiga kura wakati wa uchaguzi huo uliofanyika leo katika shule ya msingi Oysterbay, kutoka kuklia Eustace Mtumbuka,Bujiku Sakila,Amos Mwakilasa,Wilfred Mpembe,Anna Matinde na Charles Igogo ambao walichuana katika nafasi za jumla katika kundi hilo Charles Igogo na Bujiku Sakila waliibuka washindi.
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, wakiwa katika uchaguzi wa nafasi za ujumbe wa uwakilishi wa baraza la Marekebisho ya Katiba yaliyofanyika katika Mtaa huo uliopo Kata ya Msasani jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam,wakiwasikiliza baadhi ya wagombea hawapo (pichani) wa nafasi za ujumbe wa uwakilishi wa baraza la Marekebisho ya Katiba yaliyofanyika katika Mtaa huo uliopo Kata ya Msasani jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa uchaguzi katika Mtaa wa Oysterbay akitangaza matoke ya uchaguzi wa nafasi za ujumbe wa uwakilishi wa baraza la Marekebisho ya Katiba yaliyofanyika katika Mtaa huo uliopo Kata ya Msasani jijini Dar es Salaam.Picha na Mdau Albart.
No comments:
Post a Comment