Kutokana
na umamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) kupandisha nauli za usafiri wa mabasi,treni na gharama za
bandari zitakazoanza kutumika April 12 mwaka huu, usafiri wa daladala
jijini umeanza kuonekana wa shida, hasa nyakati za jioni ,kwani baadhi
ya wenye mabasi ya daladala jijini Dar es Salaam wameanza kutumia mwanya
huo na kuongeza nauli kinyemela hivyo kusababisha wananchi kutaabika na
kusongama katika vituo vya usafiri.
abiria wakisubiria usafiri kwenye kituo cha Akiba,jijin Dar.
Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam jana wakisubiri usafiri katika maeneo ya shule ya Sekondari ya Azania.
Baadhi ya wanachi katika maeneo ya Jangwani jana wakitembea kwa miguu.baada ya kuona tatizo la kususbiri usafiri.Picha na Mwanakombo Jumaa -Idara ya Habari (MAELEZO).
No comments:
Post a Comment