Wauguzi katika Hospitali ya Maweni Mkoani Kigoma wakitoa namba kwa wagonjwa waliojitokeza kuonana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Muhimbili waliopo kwenye ziara Mkoani humo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya wakina Mama Dk. Mrema (wa pili Fukuoka kulia) akimsikiliza kwa makini mmoja wa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kwa lengo la kutoa ushauri wa tiba sahihi.
Dk. Vence (Katikati) akiwa katika chumba cha upasuaji akitoa huduma kwa mmoja wa watoto ambaye alifanyiwa upasuaji mapema leo (Jumanne).
Wagonjwa wakisubiri kuonana na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Kawaida.
Akina mama wakisubiri kuonana na daktari bingwa wa akina mama.
Wagonjwa wakisubiri kuonana na daktari bingwa wa upasuaji.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee na timu ya madaktari bingwa kabla ya kuanza kazi rasmi.
No comments:
Post a Comment