HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 23, 2013

Rais Kikwete afungua mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika jijini Dar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete (Kushoto) akifungua mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika jijini Dar es Salaam jana, kikao hicho ni cha 368 na katika ajenda zake pia kitazungumzia mgogoro wa Madagascar. Pichani toka kulia ni Mjumbe wa SADC ,Joachime Chissano., Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kitaifa Mh. Bernard Membe ambae ndie Mwenyekiti wa Kikao kicho, akifuatiwa na Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika H.E. Ramatane Lamamra.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza la Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, akifungua kikao cha 368 cha baraza hilo,jijini Dar es Salaam jana,Kikao hicho ni cha siku moja ambacho pia kimehudhuliwa na Rais wa zamani wa Msumbiji ambae ni Mjumbe wa SADC hayupo pichani, (katikati) ni Kamishna wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika H.E. Ramamtane Lamamra, (kulia) ni Rais Dkt. Jakaya Kikwete.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete.
washiriki wa mkutano wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete.
baadhi ya wajumbe wa mkutano wakibadilishana mawazo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Dr. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika.Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad