Muigizaji wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi a.k.a Ray ameamua kuzungumza baada ya watu kuanza kumzushia kuwa anaumwa kutokana na kupungua kwa mwili wake kwa kiasi kikubwa hivi sasa.
Kigosi ambaye ameamua kupungua kutokana na uamuzi wake mwenye kwa kufanya mazoezi makali ili arejeshe mwili wake aliokuwa nao zamani.
Ray amejitokeza na kuzikanusha vikali tetesi zilizoanza kusambaa kwa haraka ambapo kuna moja ya gazeti la wiki hii lillkuwa na habari isemayo, "Ray apukutika mwili’ – Kitambi chote kwishnei! Ukimuona unaweza kumpita bila kumtambua, maombi ya wakatoliki yahusishwa".
"Ukweni ni kwamba nimeamua kupunguza mwili wangu kwa ridhaa yangu na wala si kwa kuumwa kama wanavyoeneza taarifa yangu."
Ray aliendelea kusema na mwisho akauliza swali “Jamani kwani unene ndio afya au kupungua ndio ugonjwa,” ameuliza Ray.
Ray yupo gado na anaendelea kupiga mzigo wake kama kawaida na hizo taarifa zinazoenezwa kusema kwamba ni mgojwa,ni uzushi mtupu.
No comments:
Post a Comment