HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 13, 2013

Mwei yazidi kunufaisha wanawake wasiokopesheka vijijini

 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (aliyebeba mtoto) akiwa katika  picha ya pamoja na wanakikundi cha Nguvu Kazi pamoja na maofisa wa Vodacom muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kukabidhi mikopo nafuu isiyo na riba wala dhamana kwa vikundi kumi vya wanwake wajasiriamali wa kata ya Kwa mndolwa vyenye wanawake wajasriamali wadogowadogo zaidi ya 90. Mikopo hiyo imetolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa Mwei.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akimsikiliza Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Salum Mwalim wakati wa hafla ya kuwapatia mikopo ya Mwei wanawake wajasiriamali zaidi ya 90 wa Kijiji cha Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe.
 Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon akiongea katika hafla ya kuwapatia mikopo ya Mwei wanawake wajasiriamali zaidi ya 90 wa Kijiji cha Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo na Meneja wa Uhusiano wa NJe wa Vodacom Salum Mwalim. Mikopo hiyo isiyo na riba wala dhamana imetolewa kwa wanawawake hao mwishoni mwa wiki kijijini hapo.
 Akina mama wajasiriamali wa kata ya Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe wakimtumbuiza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo(hayupo pichani) muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuwasili katika kijiji cha Kwa Mndolwa mwishoni mwa wiki kuongoza hafka ya kukabidhi mikopo nafuu kwa wanawake zaidi ya 90 iliyotolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa Mwei
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akiongea katika hafla ya kuwapatia mikopo ya Mwei kutoka Vodacom Foundation wanawake wajasiriamali zaidi ya 90 wa Kijiji cha Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa NJe wa Vodacom Salum Mwalim na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon (Kulia). Mikopo hiyo isiyo na riba wala dhamana imetolewa kwa wanawawake hao mwishoni mwa wiki kijijini hapo
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akimkabidhi Hadija Tengeza wa kijiji cha Kwa Mndolwa mkopo wa Mwei kutoka Vodacom Foundation uliowanufaisha wanawake wajasariamali zaidi ya 90 wa kijijini hapo. Wengine picha kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Korogwe Martha Munuo, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Afisa wa Vodacom Foundation Ally Mbuyu na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(kulia).
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim wakifuatilia maongezi na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(wa kwanza kulia) wakati Mkuu huyo na msafara wake ukiwasili katika kijiji cha Kwa Mndolwa kuongoza hafla ya utoaji mikopo ya Mwei mwishoni mwa wiki, Zaidi ya wanawake 90 wamenufaika na mikopo hiyo nafuu isiyo na riba wala dhamana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad