HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 13, 2013

JAMALI MALINZI AZUNGUMZIA KUNG'OLEWA KWAKE KUWANIA URAIS TFF

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa TFF kabla ya kuenguliwa na kamati ya uchaguzi ya TFF,Jamali Malinzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu hatua ya kuondolewa kwenye mchakato huo, ambapo alipinga kabisa hatua hiyo ya kuondolewa. Hata hivyo amemtaka Rais Tenga kumaliza vizuri kazi yake ambayo ameifanya kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kulimaliza suala hili bila ya mgogoro zaidi.

Sababu zilizotolewa na kamati ya uchaguzi ya TFF ni uzoefu wa miaka mitano, Tuhuma za kupinga waraka wa kubadili katiba ya TFF baada ya kuwekewa Pingamizi iliyowekwa na Agape Fue ambaye, alikata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya TFF kupinga kuto tendewa haki.

Alihoji kuwa huyo agape fue ni mwanamke au mwanaume kwasababu hajawahi kutokea kwenye kamati ya uchaguzi ya TFF wala kamati ya rufaa.
Waandishi wa habari mbalimbali waliojitokeza kwenye mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad