HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 20, 2013

DKT. SHEIN AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZIKO YA PADRI EVARISTUS GABRIEL MUSHI,ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, wakielekea katika Mazishi ya Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja
Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,katika kaburi alilozikwa  leo katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa
Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja
Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi ,akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja
ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita
kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana 
Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
 Baadhi ya waumini wa kanisa katoliki  wakiwa katika mazishi ya marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,
Picha na Ramadhan Othman,IKULU.

Na Maelezo Zanzibar 

 Mamia ya Wananchi wa Zanzibar leo wameshiriki Mazishi ya Padri Evaristus Mushi aliyeuwa kwa kupigwa Risasi na Watu wasiojulikana ambayo yamefanyika katika kijiji cha Kitope Wilaya ya Kaskazini B,Unguja.   Katika mazishi hayo Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad,Viongozi wa Serikali na Vyama vya siasa walihudhuria. 

 Akitoa salamu za Serikali katika Mazishi hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed alisema Serikali imeguswa sana na kifo cha Padri huyo na kuongeza kuwa itahakikisha waliohusika na tukio la mauji hayo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. 

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Anglikacana Michael hafidh amewataka Waamini wa dini ya kikristo kuwa watulivu bila kulipiza kisasi bali waiachie Serikali kufanya kazi yake ili kuwabaini waliopoteza Uhai wa Marehemu huyo. 

 Awali Mazishi hayo yalitanguliwa na Misa takatifu ya kumuombea Marehemu iliyoendeshwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam Muadhama Policarp Kadinali Pengo katika Kanisa la Minara Miwili Mjini Zanzibar. 

Padri Mushi alifariki dunia Februari 17 baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akielekea Kanisani kuendesha Misa ya Asubuhi katika Kigangwe cha Mtakatifu Teresia eneo la Beit El Raas mjini Unguja Enzi za uhai wake Padri Mushi alikuwa Msomi wa Shahada ya Uzamivu ya Elimu ya Ushauri nasaha aliyoipata nchini Marekani ambapo umauti ulimkuta akiwa anaelekea kuendesha Ibada ya Jumapili ya kwanza ya Kwarezma. 

Padri Evarist Mushi wa Kanisa la Minara Miwili mjini Zanzibar alizaliwa June 15, 1957 Mkoa wa Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa nne katika familia ya watoto sita ya Mzee Mushi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad