HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 20, 2013

NSSF yaanza kuuza Nyumba zake za Bei nafuu Kibada Kigamboni jijini Dar

Baadhi ya nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya jikoni
Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula akiangali akikagua nyumba ya shirika hilo kabla ya kuikabidhi kwa mnunuzi wa nyumba hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid.
Mmeona mandhari ya nyumba ilivyokuwa nzuri
Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula (kulia) akimkabidhi funguo ya nyumba, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid baada ya kununua nyumba ya shirika hilo iliyopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid.
Wakipewa kadi ya Luku
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid akiweka saini baada ya kununua nyumba ya shirika hilo iliyopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid. Kulia ni Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula.  
Karibuni ndani

10 comments:

  1. bei nafuu bei nafuu sema sh ngapi bhana...

    ReplyDelete
  2. bei nafuu hwo much, mbona hamsemi na mnapeanawakubwa tu,acheni kudanganya wa tz.

    ReplyDelete
  3. How much do you term as "bei nafuu"?

    ReplyDelete
  4. Wekeni bei wazi, mbona tunaona vibopa tu ndiyo wanaonunua?

    ReplyDelete
  5. Hizo nyumba ni shs ngapi? mbona matangazo hayatolewi? WATU WANAZIPATAJE? tunaomba tufahamishwe vizuri la zitaishia mikononi mwa vigogo! form za maombi ziwekwe wazi.

    ReplyDelete
  6. mauzo ya nyumba hizo hayako wazi.Ni vyema mkatangaza katika vyombo mbalimbali vya habari mkitaja bei halisi,na namna ya ulipaji.

    ReplyDelete
  7. Pls be open on this. How much does it cost for a house? Give us the categories

    ReplyDelete
  8. WEKENI BEI WAZI MBONA TUNAONA VIBOPA TU NDIYO WANAONUNUA?

    ReplyDelete

Post Bottom Ad