MSHINDI wa Bahati Nasibu ya 'Timiza Ndoto Yako, Jishindie Toyota Noah' ambayo ilikuwa inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Ramadhan Salum Pazi, mkazi wa Buguruni-Rozana jijini Dar es Salaam, leo amekabidhiwa gari lake aina ya Toyota Noah.
Makabidhiano hayo yamefanywa na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan nje ya ofisi za Global Publishers.
Bahati Nasibu hiyo iliyokuwa inaendeshwa kupitia magazeti ya Global ambayo ni Uwazi, Risasi, Championi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda ilifika mwisho Desemba 20 mwaka jana ambapo bwana Ramadhani Pazi aliibuka kidedea.
No comments:
Post a Comment