HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 3, 2013

AJALI YA RADI YAUA MTALII MMOJA MLIMA KILIMANJARO

Mgeni mmoja raia wa Ireland anayefahamika kama Ian Mc Keever amefariki dunia jana tarehe 2.1.2013 majira ya saa sita na nusu mchana  baada ya kutokea kwa ajali ya radi kali wakati akipanda Mlima Kilimanjaro akiwa pamoja na wenzake.

Ajali hiyo ya radi ilitokea katika eneo la Kibao cha Moir Hut katika njia ya Londorosi. Aidha, wageni wengine wanne walijeruhiwa katika ajali hiyo.

Marehemu Mc Keever mwenye umri wa miaka 42 alifika nchini kwa ajili ya shughuli ya utalii ya kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kampuni ya Wakala wa Utalii ya Everlasting Tour Company Limited ya Mjini Arusha ambapo marehemu pamoja na wenzake walianza safari yao ya kupanda mlima tarehe 30.12.2012

Baada ya kutokea kwa ajali hiyo wageni wengine 21 waliokuwa pamoja waliamua kuahirisha safari yao ya kupanda mlima.

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Wakala wa Utalii ya Everlasting zinaendelea na taratibu mbalimbali za kushughulikia ajali hii pamoja na matibabu kwa waliojeruhiwa.

Imetolewa na

Pascal Shelutete
Meneja Uhusiano
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad