Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa jana Jumapili jioni alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji waliofika kuaga mwili wa Marehemu Sufiani Bakari Kusaga,Nyumbani kwake Keko Maghorofani jijini Dar es salaam.
Marehemu Sufiani Bakari Kusaga alikuwa ni mume wa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Temeke ambaye sasa hivi ni Katibu wa CCM Kishapu,Mh. Khadija Kusaga.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimpa pole mfiwa,Mama Khadija Kusaga wakati alipofika nyumbani kwake Keko Maghorofani jijini Dar es salaam jana.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimfariji mfiwa,Mama Khadija Kusaga.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Mbunge wa sasa wa Jimbo la Temeke,Mh. Abbas Mtemvu wakati walipokuwa kwenye msiba huo jana jioni.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili msibani akiongozana na mwenyekiti wa CCM mkoa wa shinyanga,Hamis Mngeja.
Mwili wa Marehemu Sufiani Bakari Kusaga ukiswaliwa, kabla ya kusafirishwa kwenda Lushoto kwa mazishi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa Akisalimiana na wananchi
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Kiongozi wa zamani wa Simba,Yusuph Azali kwenye msiba wa Marehemu Sufiani Bakari Kusaga,mume wa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Temeke,Mh. Khadija Kusaga.
No comments:
Post a Comment