HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 21, 2013

Hatimae Bi Arafa Afanyiwa Upasuaji na anaendelea vema katika hospital ya Muhimbili

Kwa Niaba ya Familia ya Bi Arafa (Pichani) Napenda kutoa shukrani za Dhati kwa wale wote ambao waliguswa na hali ya Mgonjwa huyu na kuridhia kumchangia ili kumtoa wilayani Ruangwa na kuwezesha kumfikisha katika Hospital ya Muhimbili Mwezi Nov 2012 na juzi kufanyiwa Upasuaji.

Hali ya Mgonjwa huyu inaendelea vema katika hospital ya Muhimbili akisubiria kutoa Nyuzi

Mungu aliwawezesha na kumsaidia mpaka hali ilivyofikia sasa na Kubwa Nawaomba Muendelee kumuombea Dua ili aweze kupona na kuendelea kujitafutia riziki ya kila siku

Ahsanteni sana.
Ni Mimi Abdulaziz Ahmeid Video

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad