Stendi ya mabasi ya Wilaya ya Mbeya Vijijiji iliyopo eneo la Mbalizi mkoani Mbeya ambayo ilipaswa sasa kuwa katika ukarabati.lakini cha ajabu ni kwamba ukarabati wake huo umekuwa ni wakusuasua pamoja na kwamba wakazi wengi wa mji huo mdogo wa mbalizi wameiomba serikali kukamilisha kituo hicho mapema kwani tayari mvua zimeanza kunyesha na kero kubwa inaanza kutokea katika eneo hilo.
Hii ndio hali halisi ya Stendi hiyo katika eneo hilo la Mbalizi
Ukarabati wa standi hii ya Mbalizi unakuja ikiwa ni miaka mitatu tu tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete kuahidi kuikarabati Stendi hiyo baada ya kujionea na kusikiliza kilio cha wananchi waliokuwa wamejitokeza kumskiliza wakati akijinadi katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010.
Ni kipande kidogo tu mpaka sasa kimekarabatiwa katika kituo hicho cha mbalizi
Je kukakupona magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu kwa mwendo huu.......??
picha zote na Mbeya Yetu Blog.
No comments:
Post a Comment