Mwenyekiti wa Tasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania (WAMA),Mama Salma Kikwete akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vitanda 80 kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Muhimbili,Dk. Marina Njelekela.
Mwenyekiti wa Tasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania (WAMA),Mama Salma Kikwete akisoma hotuba yake mara baada ya kukabidhi vitanda 80 katika hospitali ya Muhimbili leo.kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii,Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili,Dk. Marina Njelekela.
Mwenyekiti wa Tasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania (WAMA),Mama Salma Kikwete akiongozwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Dk. Marina Njelekela (kushoto) wakati wakielekea wodini kuwatembelea wagonjwa.kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi.





Ninaomba kufafanuliwa majukumu ya Wizara ya Afya, ninadhani jukumu la kununua vitanda vya wagonjwa ni la wizara husika. Pia nimewahi kusoma kuwa WAMA wanasaidia kupambana na afya ya watoto na kinamama, kwani wizara husika haijaandaa mikakati ya kusaidia hayo yote? WAMA ni taasisi isiyo ya kiserikali, tuna uhakika gani kuwa wanawake na watoto wa nchi zima hasa vijijini watapata huduma nzuri? Serikali kupitia wizaria ya afya wanajukumu la kuhakikisha haya yote.
ReplyDeleteUtepe uliofungia vitanda mbona ni wa Taifa, kwani WAMA haina nembo yao amboyo ingetumika kuitangaza.