HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 10, 2012

uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora wafanyika mjini Lindi

Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah Mshiu (kulia) akikabidhi unga wa lishe na maziwa kwa mkazi wa Lindi, Zainabu Ali na mtoto wake Bright Abdallah, ambaye aliweza kueleza vizuri masuala ya lishe, katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi wa Save the Childern Tanzania, Rachel Pounds.
Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah Mshiu (kulia) akikabidhi zawadi ya simu ya mkononi kwa mkazi wa Lindi, Asha Mkingamila, ambaye aliweza kueleza vizuri kuliko wengine nini maana ya lishe bora , katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Save the Childern Tanzania, Rachel Pounds.
Baadhi ya watoto wa Lindi wakitembea kwa maandamano katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Shirika la Watoto la Save the Children Tanzania, Rachel Pounds, akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah Mshiu, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Hamidi Nassoro, Mbunge wa Viti Maalumu, Lediana Mafuru Mng’ong’o na Mbunge wa Serengeti, Dk Kwebe Stephen Kwebe.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Lediana Mafuru Mng’ong’o, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.
Mwanamuziki mkongwe nchini, Kassim Mapili, akifanya vitu vyake pamoja na wasanii wa Mjomba Band, katika hafla ya katikasherehe za uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.
Msanii wa Mashairi, Mrosho Mpoto, akikonga nyoyo za wakazi wa Lindi waliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad