HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 10, 2012

Maadhimisho ya Siku ya Haki za binadamu

Mgeni Rasmi wa kilele cha Maadhimisho ya Haki za Binadamu na Kupambana na Kuzuia rushwa Mhe. Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha mifumo ya habari na mawasiliano ya kompyuta Bw. Wilfred Warioba katika Banda la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuhusu kazi za Tume na Mfumo mpya wa kuwasilisha malalamiko mbele ya Tume kwa kutumia ujumbe wa simu ya Kiganjani katika viwanja vya mnazi mmoja mapema leo.
Wageni mbali mbali wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha mifumo ya habari na mawasiliano ya kompyuta Bw. Wilfred Warioba katika banda la THBUB siku ya Maadhimisho ya Haki za Binadamu na Kupambana na Kuzuia rushwa yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja mapema leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Jaji kiongozi (mstaafu) Amiri R. Manento akihutubia siku ya Haki za Binadamu na Kuzuia na kupambana na Rushwa katika viwanja vya mnazi mmoja. mapema leo.(picha na Mbaraka Kambona).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad