HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 10, 2012

Francis Miyeyusho amtandika Nassib Ramadhan kwa t.k.o

Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akimvisha mkanda wa ubingwa wa WBF,bondia Francis Miyeyusho baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani kwa T.K.O raundi ya kumi.kushoto ni promota wa mpambano huo,Mohamed Bawazir.
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akimpongeza Bingwa wa WBF,bondia Francis Miyeyusho baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani  kwa T.K.O raundi ya kumi.kushoto ni promota wa mpambano huo Mohamed Bawazir.
Bondia Fransic Miyeyusho (kulia) akionesha ufundi wake kwa kumtupia masumbwi Bondia mwenzie,Nassibu Ramadhani wakati wa Mpambano wao wa kuwania ubingwa wa WBF uliofanyika jana jioni kwenye Ukumbi wa PTA,Sabasaba jijini Dar es Salaam.Miyeyusho alishinda mchezo huo kwa T.K.O raundi ya kumi.
Bondia Francis Miyeyusho (kushoto) akimpatia dozi za kutosha mpinzani wake,Nassibu Ramadhani wakati wa Mpambano wao wa kuwania ubingwa wa WBF uliofanyika jana jioni kwenye Ukumbi wa PTA,Sabasaba,Jijini Dar es Salaam.Miyeyusho alishinda kwa T.K.O raundi ya kumi.
bondia Francis Miyeyusho akiwa amebebwa juu juu na mashabiki wake huku akiwa na mikanda yake miwili aliyoshinda baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani.
Mdau wa Mchezo wa Masumbwi,Rajabu Mhamila (kushoto) akiwa na wadau waliojitokeza kuangalia mpambano huo.Picha na Super D Boxing 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad