HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 13, 2012

SPIKA MAKINDA AFUNGUA MKUTANO WA CHAMA CHA WABUNGE WA JUMUIYA YA MADOLA JIJINI ARUSHA

Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Parliamentary Association - CPA) Kanda ya Afrika. Spika Makinda pia ni Makamu wa Rais wa CPA Kanda ya Afrika. Chama hicho cha Wabunge kiko katika Mabunge ya Nchi 19 na Mabaraza ya Kutunga Sheria 45 barani Afrika. Mkutano wa Kamati ya Uongozi hukutana kila mwisho wa mwaka kuangalia mwenendo wa kimkakati (strategic direction) na kupitisha maamuzi makubwa ambayo yanahitaji utekelezaji wa haraka. Kulia ni Spika wa Malawi na Mwakilishi wa CPA Kanda Ndogo ya Afrika ya Kati, Mhe. Henry Chimunthu Banda.
Spika wa Bunge Anne Makinda akipokea zawadi toka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Barani Afrika, Spika Lindiwe Maseko wa Jimbo la Gauteng,Afrika Kusini huku wakishuhudiwa na Makatibu wa Mabunge hayo, Dr. Thomas Kashililah (kwanza kulia) wa Tanzania na Peter Skosana wa Jimbo la Gauteng. Spika Maseko yuko nchini kuhudhuria Mkutano wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola.
Picha ya pamoja ya Washiriki wa Mkutano wa Kamati ya Uongozi ya CPA Barani Afrika na Sekretarieti yake unaofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. PICHA KWA HISANI YA OFISI YA BUNGE

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad