Katika pita pita zangu za kila siku,nikaibukia hapa Mikocheni ku kwenye kituo cha Dala Dala cha Chama ambapo ni Usoni kabisa mwa jengo la Tanesco Wilaya ya Kinondoni.Nilipatwa na Mshangao baada ya kuwaona Wanyama hawa aina ya Kondoo wakiwa nje ya jengo hilo huku wakipiga msosi chapa mchanga na wakionekana hawana noma wala nini.sasa sijui kuna mtu kaja nao na kuwaacha nje,ili yeye aweze kuwahi kununua Luku au ndio kila kiumbe kwa raha zake.
Tuesday, November 27, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WANYAMA KUONEKANA MAENEO WA MIJINI NI JAMBO LA KAWAIDA HASA MAENEO YA PWANI MFANO MJINI TANGA MIAKA YA SABINI KULIKUWA NA MBUZI WAKIZURURA STEND YA MAGARI WAKIPISHA MAGARI BILA KUGONGWA UKIULIZA INADAIWA WALIIBIWA WAKASOMEWA AL BADIR WALIOWAIBA WAKAJA WAKAWAACHA MJINI SIJUI KUNA UKWELI
ReplyDelete