HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 27, 2012

JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge BCBG wawasili jijini dar usiku huu

Mwanamuziki nguli wa dansi Barani Afrika, JB Mpiana (mwenye kofia) akiongoza na baadhi ya wenyeji wake pamoja na wanamuziki wa Bendi yake ya Wenge BCBG wakati wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam usiku huu. JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge BCBG wanatarajiwa kufanya Onyesho moja kubwa jijini Dar,Novemba 30,2012 kwenye Viwanja vya Leaders,Kinondoni jijini Dar.
Mwanamuziki nguli wa dansi Barani Afrika, JB Mpiana (mwenye kofia) akiongoza na Mwanamuziki mwingine Mkongwe hapa nchini,Ndanda Kosovo (mwenye shati nyeupe) wakati akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam usiku huu.
Mwanamuziki nguli wa dansi Barani Afrika, JB Mpiana akifanya mahojiano na Baadhi ya Waandishi wa Habari waliofika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam usiku huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad