HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 8, 2012

Zuku Tunakuthamani - Pata TV Bure Yazinduliwa

Meneja msaidizi masoko Zuku,Veranda Raphael akielezea kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwazawadia wateja ya Tunakuthamini Zuku - Pata TV Bure Programu. hii itawazawadia wateja ambao wataunganisha wateja wapya kwa mtandao wa Zuku. Katikati ni Irene Muratha, Mkuu wa Masoko Wananchi Satellite na Fadhili Mwasyeba Meneja Wananchi SaelliteTanzania.
Meneja Wananchi Satellite Tanzania,Fadhili Mwasyeba (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mtandao wa mawakala wa Zuku wakati wa uzinduzi wa programu ya kuzawadia wateja ya Zuku Tunakuthamini - Pata TV Bure. Programu hii itawazawadia wateja ambao wataunganisha wateja wapya kwa mtandao wa Zuku. Kulia ni Veranda Raphael Assitant wa Zuku.

Zuku inayomilikiwa na kampuni ya Wananchi, imezindua programu ya kuwazawadia wateja wao ya Zuku Tunakuthamini – Pata TV Bure jijini Dar es Salaam. Zuku Satellite Pay TV ni king'amuzi cha burundani cha televisheni ambacho kinachanneli zaidi ya 70. 

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Irene Muratha Mkuu wa Masoko ya Wananchi Satellite alibainisha kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambayo uchumi wake unakukua kwa kasi katika Afrika Mashariki na kampuni ya Wananchi Group - kampuni inayomiliki Zuku Satellite Pay TV- ni miongoni mwa wawekezaji katika nchi hii. 

Aliongeza kuwa, "Tangu uzinduzi wa Zuku Satellite Pay TV mapema kwa mwaka, tunaendelea kuwekeza nchini na udhamini wetu wa ZIFF ambayo inaweka filamu za tanzania kwenye jukwaa la kimataifa, Hyped East Afrika na leo hii tunazindua uwekezaji wetu mpya wa programu ya Zuku Tunakuthamini - Pata TV Bure. 

 Programu hii ya kuwazawadia wateja, itahitaji kuungananisha wateja kumi (10) au kuunganisha wateja watano (5) wateja wapya na kupata uhakika wa kushinda televisheni ya inchi 42 na inchi 22. Programu hii ni ya kipekee kwa kuwa wateja wote ambao watakaohudhuria wanauhakika wa kushinda tena na tena. 

Programu hii itaendelea hadi Desemba 31, 2012. Veranda Raphael, Msaidizi Masoko Zuku Tanzania, alielezea kuwa programu hii ni kwa wateja waliopo na wateja wapya ambao watashiriki.

 Vigezo na masharti zinapatikana kwa wakala wote wa Zuku nchini.

Zuku TV inatoa uchaguzi mpana wa burudani, habari, michezo, sinema, na dini na muziki. Zuku pia inamiliki channeli kam vile Zuku Afrika, Zuku Movies, Zuku Sports na Zuku Action. King'amuzi cha Zuku kinapatikana kote nchini katika mawakala wake  na kujiunga ni Ths 92,000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad