Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB Bw. Imani Kajula (kushoto)
akitoa ufafanuzi wa promosheni mpya ya Ki-College zaidi kwa viongozi wa
vyuo vya elimu ya juu waliohudhuria uzinduzi huo wikiendi hii.
Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Idara ya wateja binafsi wa NMB Bw. Abdulmajid
Nsekela,(pili kushoto) Makamu wa Rais wa chuo cha DUCE, Bi. Kagema Ftain
na Makamu wa Rais wa Chuo cha Ardhi Bw. Stephen Mokare.
Viongozi
wa Vyuo mbali mbali vya elimu ya juu wakiwa kwenye picha ya pamoja na
wafanyakazi wa NMB wakati wa uzinduzi wa kampeni ya NMB Student Account
iitwayo Ki COLLEGE zaidi na NMB, hafla hiyo ilifanyika wikiendi hii
jijini Dar es Salaam.
NMB
ndiyo Benki yenye mtandao mpana wa matawi na ATM nyingi zaidi nchini na
imekuwa kinara katika ubunifu Tanzania kwa kuanzisha akaunti
zinazokidhi matakwa ya wateja mbalimbali.
Kwa
kutambua jambo hili mwaka 2007, Benki ya NMB ilianzisha akaunti maalumu
kwa ajili ya wanafunzi iitwayo NMB Student Account. Akaunti hii
ilianzishwa ili kuwawezesha wanafunzi kupata huduma za kibenki kwa
urahisi na unafuu zaidi.
Ki-COLLEGE
zaidi na NMB ni promosheni inayowawezesha wanafunzi wenye akaunti ya
NMB Student Account kupata nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia
Zawadi mablimbali kama: iPad, Samsung Galaxy, Amana maradufu, flash
disk, fulana za NMB, taa inayotumia mionzi ya jua au amana maradufu. Ili
uweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia zawadi kwenye
promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na NMB, fungua NMB Student Account, weka
amana katika akaunti yako, tumia au jiunge na NMB mobile .
Ikiwa
hujatumia akaunti yako kawa muda mrefu tembelea tawi la NMB ili nawe
ushiriki katika promosheni hii ya ki-COLLEGE zaidi na NMB.
Pamoja na kampeni hii, wanafunzi watakao fungua NMB Student Account
wataendelea kufurahia huduma za NMB Student Account kama:
Kufungua
akaunti kwa Sh. 10,000 tu (pamoja na NMB ATM kadi),kujiunga na huduma
ya NMB mobile bure kupata huduma ya ujumbe mfupi kila utoapo fedha
kwenye ATM ya NMB bure, kuchukua fedha hadi Sh.1,000,000 kwenye NMB ATM
kwa siku na kupata huduma kupitia matawi zaidi ya 143 na NMB ATM zaidi
ya 450 nchi nzima.
Kampeni ya ki-COLLEGE zaidi na NMB iliyoanza rasmi Oktoba 1 itaendelea
hadi Desemba 31, 2012.
No comments:
Post a Comment